Mganga wa mfumo wa taarifa za uendeshaji wa huduma za afya (MTUHA) wa Hospitali ya rufaa mkoa wa Ruvuma Michael Hyera amesema kuwa jumla ya watoto arobaini na nane wenye umri chini ya miaka mitano wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa maralia tangu mwezi january hadi mwezi june mwaka huu 2013.
Amesema takwimu za vifo hivyo kwa watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa mwaka jana.
Kwa upande mwingine amesema kuwa jamii haina budi kutumia vyandarua kila siku katika familia zao na kuhakikisha wanasafisha mazingira ili kuzuia mazalia ya mbu.
Mstahiki meya wa manispaa ya Songea Charles Mhagama amewataka wananchi kushirikiana na viongozi katika shughuli za kuboresha miradi mbalimbali katika jamii ikiwemo ujenzi wa shule,nyumba za walimu na zahanati.
Amesema kuwa manispaa kwa kulitaza suala hilo imeanza ujenzi wa maabara na nyumba za walimu katika shule ya sekondari mdandamo na shule ya sekondari ya subiri.
Kwa upande mwingine amesema kuwa zoezi la kuboresha miradi mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya manispaa ni endelevu.
Diwani wa kata ya peramiho iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya songea vijijini Izack mwimba amewataka wananchi wa vijiji ambavyo vinapitiwa na umeme wa greedi ya taifa kujianda kwa kujenga nyumba za bati ili kunufaika na mradi huo kutoka shirika la umeme kwa kushirikina na ufadhiri wa serikali ya Swideni SIDA.
Amesema kutokana na maelekezo yalitotelewa na shirika la umeme kuwa mradi huo unaanza mwezi januari 2014 hivyo muda huo siyo mwingi kwani kutokuweka mazingira vizuri yanaweza kusababisha wanachi kutonufaika na mradi huo.
Ameongeza kuwa serikali imeamua kuboresha huduma hiyo hivyo wanachi hawana budi kuweka mazingira mazuriili kupata mradi huo ndani ya miezi kumi nane kama ilivyopangwa na serikli kwa kushirikiana na serikali ya Swideni.
Hayo ameyazungumza katika kijiji cha Lundusi ikiwa ni moja kati ya 5 vya kata ya peramiho ambavyo vitanufaika na mradi huo wa umeme kwa greedi ya taifa.
Imechapishwa kwa msaada wa JOGOO FM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni