Wananchi ya kijiji cha Lundusi kilichopo kata ya peramiho halmashauri ya wilaya ya songea vijiji wamelitaka shirika la umeme nchini kusambaza umeme kwa GREEDI ya taifa kwa muda muafaka wa miezi kumi na nane katika vijiji 54 vya mkoa wa Ruvuma ili kusaidia kuinua maendeleo vijini.
Wamesema kuwepo kwa nishati hiyo ya umeme kutasaidia kutoa fursa za ajira kwa vijana huku wakibainsha licha kuwepo kwa fursa ya ajira lakini maendeleo ya maeneo hayo yatakua ukichukulia na sasa ambapo hawana nishati ya umeme.
Wameongeza kuwa ili kunufaika na mpango huo wa serikali kwa kushirikiana na serikali ya Swideni (SIDA) wamejipanga kikamilifu kwa kujenga nyumba za bati na kufunga nyaya katika nyumba zao kuanzia sasa mpaka kufikia miezi hiyo 18 ya mradi huo kukamilika.
Katibu wa chama cha TADEA Mkoa wa Ruvuma Peter Charles amevitaka vyama vya siasa ambavyo vimepinga kusainiwa kwa mswada wa rasimu ya katiba mpya kukaa pamoja na serikali ili kuweza kutatua tatizo hilo na sio kupinga.
Amesema kuwa vyama hivyo havina budi kutambua kuwa katiba itawawezesha wananchi kujua taratibu mbalimbali za nchi ambazo zitawanufaisha watanzania na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake katibu wa chama cha UDP mkoa wa ruvuma Richard Tawe amesema kuwa vyama hivyo vitambue kuwa katiba ndio maisha ya watanzania hivyo kuundwa kwa katiba mpya kutasaidia kuwakomboa wananchi kwa kujua haki zao katika jamii.
Wamesema hayo kufuatia ushirikiano wa baadhi ya vyama vya Upinzani nchini, kumtaka Rais Jakaya Kikwete kwamba asisahini Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge mjini Dodoma hivi karibuni na tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Freeman Mbowe wa Chama na mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
Imechapishwa kwa msaada wa JOGOO FM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni