Katibu wa soko la mazao sodeko lilipo manispaa ya songea Tadei Mwakaguo amewataka wakulima na wafanyabiashara wa mazao kujiunga katika sacos ambazo watazitumia kuhifadhi na kukopa fedha za kuendeleza shughuli za kilimo.
Amesema umoja wa wakulima wa soko hilo (UWAMAVIRU) wameanzisha chama cha sacos ambacho kinajumla ya wanachama mia moja na amewaomba wakulima wengine kutumia vyama hivyo ambavyo vitaweza kuwarahisishia maendeleo yao.
Kwa upande wa wakulima ambao wamejiunga katika sacos hiyo wanasema kuwa moja ya faida ya kutumia sacos ni kuweza kuwasogezea wakulima huduma karibu kwa kuwa watatumia kuhifadhi fedha na kukopa ili kukuza mitaji yao.
Soko la sodeko ni soko ambalo limeanzishwa mwaka 1995 na kupata usajili wake mwaka 2003 na lengo lake likiwa ni kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao.
Afisa mkuu huduma kwa wateja shrika la umeme Tanzania Musa chgowo amesema sababu za kusambaza umeme kwa gredi ya taifa mkoa wa Ruvuma lengo ni kusogeza huduma ya shirika hilo kwa wananchi wake.
Amesema kuwa huduma hiyo itahudumia zaidi ya vijiji 80 vya mkoa wa Ruvuma huku mradi unaotarajia kusambaza umeme huo ni ule wa makambako songea na mkondo wa kusambaza umewme utafungwa manispaa ya songea ili kusambaza katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma.
Ameongeza kuwa kutokana na huduma hiyo ya greedi ya taifa gharama za kusambaza umeme kwa wananchi zitapungua kutoka laki 3 hadi laki 5 mpaka elfu 32,900 kwa wanachi watahitaji kipindi cha mradi huo.
Mradi wa makambako songea ambao utasambaza umeme kwa greedi ya taifa utakamilika ndani ya miezi kumi na nane na utasambazwa kwa kushirikiana na shirika la SWIDENI(SWIDA)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni