Jumanne, 1 Oktoba 2013

TANZANIA MAMBO VIPI??

Ni kijana wa kitanzania mwenye lengo la kukuhabarisha taarifa mbalimbali mchangie mawazo yako ili asonge zaidi.

SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA MOSI 2013

Oktoba mosi kila mwaka wazee Tanzania huungana na wazee wenzao duniani kote kuadhimisha siku ya wazee duniani, ambapo hutumia siku hiyo kuwasilisha hoja, kero na hisia zao kwa serikali juu ya masuala mbalimbali.


Maadhimisho ya siku hii huambatana na kauli mbiu mbalimbali ambazo huwa na lengo la kuelezea masuala kadhaa yanayohusu mustakabali wao katika maisha yao ya uzeeni katika nchi husika.

Kwa Tanzania Sera ya taifa ya afya na sheria ya utumishi wa umma inazingatia umri ya miaka 60 kuwa ndio kigezo cha uzee kwani nguvu za kufanya kazi zinakuwa zimepungua.

Aidha wazee nchini wamegawanyika katika makundi mbalimbali, ambapo lipo kundi ya wazee wastaafu, wazee wakulima, wafugaji, wavuvi na wazee wasio na ajira, makundi yote ya wazee yanatofautiana kimatatizo na kimahitaji kutoka kundi moja hadi jingine.

Kwa Tanzania Sera ya taifa ya afya na sheria ya utumishi wa umma inazingatia umri ya miaka 60 kuwa ndio kigezo cha uzee kwani nguvu za kufanya kazi zinakuwa zimepungua.   

TAARIFA ZAIDI KUTOKA KWA WAZEE WA SONGEA  ZITAKUJIA BAADAE.


Jumapili, 22 Septemba 2013

KUTOKA SONGEA.

Mganga  wa mfumo wa taarifa za uendeshaji  wa huduma za afya (MTUHA) wa Hospitali ya rufaa mkoa wa Ruvuma Michael Hyera amesema kuwa jumla ya watoto arobaini na nane wenye umri chini ya miaka mitano wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa maralia tangu mwezi january hadi mwezi june  mwaka huu 2013.
Amesema takwimu za vifo hivyo kwa watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa mwaka jana.
Kwa upande mwingine amesema kuwa jamii haina budi kutumia vyandarua kila siku katika familia zao na kuhakikisha wanasafisha mazingira  ili kuzuia mazalia ya mbu.


Mstahiki meya wa manispaa ya Songea Charles Mhagama amewataka wananchi kushirikiana na viongozi katika  shughuli za kuboresha miradi mbalimbali katika jamii ikiwemo ujenzi wa shule,nyumba za walimu  na zahanati.
Amesema kuwa manispaa kwa kulitaza suala hilo imeanza ujenzi wa maabara na nyumba za walimu katika shule ya sekondari mdandamo na shule ya sekondari ya subiri.
Kwa upande mwingine amesema kuwa zoezi la kuboresha miradi mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya manispaa ni endelevu.


Diwani wa kata ya peramiho iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya songea vijijini Izack mwimba amewataka wananchi wa vijiji ambavyo vinapitiwa na umeme wa greedi ya taifa kujianda kwa kujenga nyumba za bati ili kunufaika na mradi huo kutoka shirika la umeme kwa kushirikina na ufadhiri wa serikali ya Swideni SIDA.
Amesema kutokana na maelekezo yalitotelewa na shirika la umeme kuwa mradi huo unaanza mwezi januari 2014 hivyo  muda huo siyo mwingi kwani kutokuweka mazingira vizuri yanaweza kusababisha wanachi kutonufaika na mradi huo.
Ameongeza kuwa serikali imeamua kuboresha huduma hiyo hivyo wanachi hawana budi kuweka mazingira mazuriili  kupata mradi huo ndani ya miezi kumi nane kama ilivyopangwa na serikli kwa kushirikiana na serikali ya Swideni.
Hayo ameyazungumza katika kijiji cha Lundusi ikiwa ni moja kati ya 5 vya kata ya peramiho ambavyo vitanufaika na mradi huo wa umeme kwa greedi ya taifa.
 

Imechapishwa kwa msaada wa JOGOO FM.
 

HABARI KUTOKA SONGEA

Wananchi ya kijiji cha Lundusi kilichopo kata ya peramiho halmashauri ya wilaya ya songea vijiji wamelitaka shirika la umeme nchini kusambaza umeme kwa GREEDI ya taifa kwa muda muafaka wa miezi kumi na nane katika vijiji 54 vya mkoa wa Ruvuma ili kusaidia kuinua maendeleo vijini.
Wamesema kuwepo kwa nishati hiyo ya umeme kutasaidia kutoa fursa za ajira kwa vijana huku wakibainsha licha kuwepo kwa fursa ya ajira lakini maendeleo ya maeneo hayo yatakua ukichukulia na sasa ambapo hawana nishati ya umeme.
Wameongeza kuwa ili kunufaika na mpango huo wa serikali kwa kushirikiana na serikali ya Swideni (SIDA) wamejipanga kikamilifu kwa kujenga nyumba za  bati na kufunga nyaya katika nyumba zao kuanzia sasa mpaka kufikia miezi hiyo 18 ya mradi huo kukamilika.



Katibu wa chama cha TADEA Mkoa wa Ruvuma Peter Charles amevitaka vyama vya siasa ambavyo vimepinga kusainiwa kwa mswada wa rasimu ya katiba mpya kukaa pamoja na serikali ili kuweza kutatua tatizo hilo na sio kupinga.
Amesema kuwa vyama hivyo havina budi kutambua kuwa katiba itawawezesha wananchi kujua taratibu mbalimbali za nchi ambazo zitawanufaisha  watanzania na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake katibu wa chama cha UDP mkoa wa ruvuma  Richard Tawe amesema kuwa vyama hivyo vitambue kuwa katiba ndio maisha ya watanzania hivyo kuundwa kwa katiba mpya kutasaidia kuwakomboa wananchi kwa kujua haki zao katika jamii.
Wamesema hayo kufuatia ushirikiano wa baadhi ya  vyama vya Upinzani nchini, kumtaka Rais Jakaya Kikwete kwamba asisahini  Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge mjini Dodoma hivi karibuni na tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia, mwenyekiti  wa Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Freeman Mbowe wa Chama na mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba. 








Imechapishwa kwa msaada wa JOGOO FM.

Jumamosi, 14 Septemba 2013

HABARI KUTOKA SONGEA

Katibu wa soko la mazao sodeko lilipo manispaa ya songea Tadei Mwakaguo amewataka wakulima na wafanyabiashara wa mazao kujiunga katika sacos ambazo watazitumia kuhifadhi na kukopa fedha za kuendeleza shughuli za kilimo. 
Amesema umoja wa wakulima wa soko hilo (UWAMAVIRU) wameanzisha chama cha sacos ambacho kinajumla ya wanachama mia moja na amewaomba wakulima wengine kutumia vyama hivyo ambavyo vitaweza kuwarahisishia maendeleo yao.
Kwa upande wa wakulima ambao wamejiunga katika sacos hiyo wanasema kuwa moja ya faida ya kutumia sacos ni kuweza kuwasogezea wakulima huduma karibu kwa kuwa watatumia kuhifadhi fedha na kukopa ili kukuza mitaji yao.
Soko la sodeko ni soko ambalo limeanzishwa mwaka 1995 na kupata usajili wake mwaka 2003 na lengo lake likiwa ni kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao.






 

Afisa mkuu huduma kwa wateja shrika la umeme Tanzania Musa chgowo amesema sababu za kusambaza umeme  kwa gredi ya taifa mkoa wa Ruvuma lengo ni kusogeza huduma ya shirika hilo kwa wananchi wake.
Amesema kuwa huduma hiyo itahudumia zaidi ya vijiji 80 vya mkoa wa Ruvuma huku mradi unaotarajia kusambaza umeme huo ni ule wa makambako songea na mkondo wa kusambaza umewme utafungwa manispaa ya songea ili kusambaza katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma.
Ameongeza kuwa kutokana na huduma hiyo ya greedi ya taifa gharama za kusambaza umeme kwa wananchi zitapungua kutoka laki 3 hadi laki 5 mpaka elfu 32,900 kwa wanachi watahitaji kipindi cha mradi huo.
Mradi wa makambako songea ambao utasambaza umeme kwa greedi ya taifa utakamilika ndani ya miezi kumi na nane na utasambazwa kwa kushirikiana na shirika la SWIDENI(SWIDA)

Jumamosi, 17 Agosti 2013

KIMATAIFA

BADO  TUNAENDELEA NA MAREKEBISHO BAADA YA MUDA MFUPI UTAANZA KUFURAHIA HABARI ZA UHAKIKA.