Jumanne, 17 Juni 2014

BREAKING NEWSSSSSSSSSSS

Wanafunzi 54,085 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano  mwaka huu, watakiwa kuripoti Julai  10. Taarifa kutoka kwa Naibu Waziri Tamisemi (Elimu) Kassim Majaliwa.

Jumatatu, 16 Juni 2014

BREAKING NEWSSSSS


Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kaskazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi ya pili.Katika tukio jengine kundi la Taleban limewakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.

BREAKING NEWSSSSSS

Raia wazingira Zahanati Kaijara, Muleba wakidai mwili wa mtoto aliyerudishwa  kutoka Arusha baada ya kupoteza maisha umenyofolewa baadhi ya viungo.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye amekatwa titi na sehemu za siri alikuwa akifanya kazi za ndani mkoani Arusha kabla hajapatwa na mauti. Polisi wanakabiliana na raia hao huku wakiwaomba wamsubiri daktari afanye uchunguzi kwanza.
Katika hatua nyingine raia wamefanikiwa kuvunja Zahanati  na kuukuta mwili wa binti huyo umeng'olewa meno, kutobolewa tumbo. Ripota wa mwananchi anayefuatili tukio hilo apigwa na polisi.

TAARIFA ZAIDI TUTAKUJUZA KITAKACHOENDELEA: ASANTE KWA KUTUCHAGU

BREAKING NEWSSSSS

Watu 48 wapoteza maisha katika shambulio nchini Kenya Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha. Taarifa ambayo ilitolewa awali na jeshi nchini Kenya  ilitangazwa kwamba ni watu 26 ndio wamepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo limetokea katika hoteli mbili  mjini Mpeketoni.