Jumanne, 17 Juni 2014

BREAKING NEWSSSSSSSSSSS

Wanafunzi 54,085 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano  mwaka huu, watakiwa kuripoti Julai  10. Taarifa kutoka kwa Naibu Waziri Tamisemi (Elimu) Kassim Majaliwa.

Jumatatu, 16 Juni 2014

BREAKING NEWSSSSS


Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kaskazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi ya pili.Katika tukio jengine kundi la Taleban limewakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.

BREAKING NEWSSSSSS

Raia wazingira Zahanati Kaijara, Muleba wakidai mwili wa mtoto aliyerudishwa  kutoka Arusha baada ya kupoteza maisha umenyofolewa baadhi ya viungo.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye amekatwa titi na sehemu za siri alikuwa akifanya kazi za ndani mkoani Arusha kabla hajapatwa na mauti. Polisi wanakabiliana na raia hao huku wakiwaomba wamsubiri daktari afanye uchunguzi kwanza.
Katika hatua nyingine raia wamefanikiwa kuvunja Zahanati  na kuukuta mwili wa binti huyo umeng'olewa meno, kutobolewa tumbo. Ripota wa mwananchi anayefuatili tukio hilo apigwa na polisi.

TAARIFA ZAIDI TUTAKUJUZA KITAKACHOENDELEA: ASANTE KWA KUTUCHAGU

BREAKING NEWSSSSS

Watu 48 wapoteza maisha katika shambulio nchini Kenya Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha. Taarifa ambayo ilitolewa awali na jeshi nchini Kenya  ilitangazwa kwamba ni watu 26 ndio wamepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo limetokea katika hoteli mbili  mjini Mpeketoni.

Jumapili, 25 Mei 2014

TANGAZO KWA WATEMBELEAJI

HABARI WATEMBELEAJI WA BLOG HII, TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA SIKU CHACHE KUTOKA SASA UTAWEZA KUSOMA HABARI MBALIMBALI ZILIZOCHAMBULIWA NA KUHARIRIWA NA WANAHABARI WALIOBOBEA KATIKA TASNIA YA HABARI.

SAMAHANI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA SIKU ZA NYUMA.




UKWELI NA UHAKIKA

Ijumaa, 17 Januari 2014



MFAHAMU MWANAMAPINDUZI CHE GUAVARA.

Ernesto Rafael Guevara de la Serna au Che Guevara  alizaliwa tarehe 14. Mei 1928 Rosario, Argentina;  9. Oktoba 1967 La Higuera, Bolivia alikuwa mtabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi.
Aliamua kusoma kwa undani falsafa za Karl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za kisoshalisti nchini Guatemala chini ya rais Jacobo Arbenzi Guzmán.Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la kijeshi lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini Cuba mwaka 1959. Guevara alikuwa mmoja wa viongozi wa serikali mpya ya Cuba. Katika kipindi hiki, Guevara aliandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita vya msituni kwa nia ya kuondoa madarakani tawala za kibepari na kibeberu.Mwaka 1965 Guevara aliondoka nchini Cuba akielekea Kongo-Kinshasa ambayo hivi sasa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa siri kusaidia harakati za kuondoa utawala uliokuwa ukiongozwa na vibaraka wa mataifa ya Magharibi chini ya Mobutu Sese Seko
baada ya kuuawa kwa Patrice Lumumba. Moja ya watu ambao walifanya kazi na Guevara alipokuwa nchini Kongo ni aliyekuwa baadaye  rais wa nchi hiyo, Laurent Kabila.
Guevara aliondoka nchini Congo na kuelekea Bolivia ambapo alikamatwa mwaka 1967 na jeshi la Bolivia likishirikiana na majasusi wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA. Baada ya kukamatwa kwake aliuawa kinyama.
Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda kuivaa vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.

Imechapishwa kwa msaada kwa msaada Wikipedia

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA JULAI 2014 HAYA HAPA