Jumanne, 1 Oktoba 2013

TANZANIA MAMBO VIPI??

Ni kijana wa kitanzania mwenye lengo la kukuhabarisha taarifa mbalimbali mchangie mawazo yako ili asonge zaidi.

SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA MOSI 2013

Oktoba mosi kila mwaka wazee Tanzania huungana na wazee wenzao duniani kote kuadhimisha siku ya wazee duniani, ambapo hutumia siku hiyo kuwasilisha hoja, kero na hisia zao kwa serikali juu ya masuala mbalimbali.


Maadhimisho ya siku hii huambatana na kauli mbiu mbalimbali ambazo huwa na lengo la kuelezea masuala kadhaa yanayohusu mustakabali wao katika maisha yao ya uzeeni katika nchi husika.

Kwa Tanzania Sera ya taifa ya afya na sheria ya utumishi wa umma inazingatia umri ya miaka 60 kuwa ndio kigezo cha uzee kwani nguvu za kufanya kazi zinakuwa zimepungua.

Aidha wazee nchini wamegawanyika katika makundi mbalimbali, ambapo lipo kundi ya wazee wastaafu, wazee wakulima, wafugaji, wavuvi na wazee wasio na ajira, makundi yote ya wazee yanatofautiana kimatatizo na kimahitaji kutoka kundi moja hadi jingine.

Kwa Tanzania Sera ya taifa ya afya na sheria ya utumishi wa umma inazingatia umri ya miaka 60 kuwa ndio kigezo cha uzee kwani nguvu za kufanya kazi zinakuwa zimepungua.   

TAARIFA ZAIDI KUTOKA KWA WAZEE WA SONGEA  ZITAKUJIA BAADAE.