ANTONY KOMBA
Jumanne, 17 Juni 2014
BREAKING NEWSSSSSSSSSSS
Wanafunzi 54,085 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, watakiwa kuripoti Julai 10. Taarifa kutoka kwa Naibu Waziri Tamisemi (Elimu) Kassim Majaliwa.
Jumatatu, 16 Juni 2014
BREAKING NEWSSSSS
Maafisa nchini Afghanistan
wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi
baada ya gari lao kaskazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa
barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi
ya pili.Katika tukio jengine kundi la Taleban limewakata vidole baadhi
ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.
BREAKING NEWSSSSSS
Raia wazingira Zahanati Kaijara, Muleba wakidai mwili wa mtoto aliyerudishwa kutoka Arusha baada ya kupoteza maisha umenyofolewa baadhi ya viungo.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye amekatwa titi na sehemu za siri alikuwa akifanya kazi za ndani mkoani Arusha kabla hajapatwa na mauti. Polisi wanakabiliana na raia hao huku wakiwaomba wamsubiri daktari afanye uchunguzi kwanza.
Katika hatua nyingine raia wamefanikiwa kuvunja Zahanati na kuukuta mwili wa binti huyo umeng'olewa meno, kutobolewa tumbo. Ripota wa mwananchi anayefuatili tukio hilo apigwa na polisi.
TAARIFA ZAIDI TUTAKUJUZA KITAKACHOENDELEA: ASANTE KWA KUTUCHAGUA
Binti huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye amekatwa titi na sehemu za siri alikuwa akifanya kazi za ndani mkoani Arusha kabla hajapatwa na mauti. Polisi wanakabiliana na raia hao huku wakiwaomba wamsubiri daktari afanye uchunguzi kwanza.
Katika hatua nyingine raia wamefanikiwa kuvunja Zahanati na kuukuta mwili wa binti huyo umeng'olewa meno, kutobolewa tumbo. Ripota wa mwananchi anayefuatili tukio hilo apigwa na polisi.
TAARIFA ZAIDI TUTAKUJUZA KITAKACHOENDELEA: ASANTE KWA KUTUCHAGUA
BREAKING NEWSSSSS
Watu 48 wapoteza maisha katika shambulio nchini Kenya Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha. Taarifa ambayo ilitolewa awali na jeshi nchini Kenya ilitangazwa kwamba ni watu 26 ndio wamepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo limetokea katika hoteli mbili mjini Mpeketoni.
Jumapili, 25 Mei 2014
TANGAZO KWA WATEMBELEAJI
HABARI WATEMBELEAJI WA BLOG HII, TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA SIKU CHACHE KUTOKA SASA UTAWEZA KUSOMA HABARI MBALIMBALI ZILIZOCHAMBULIWA NA KUHARIRIWA NA WANAHABARI WALIOBOBEA KATIKA TASNIA YA HABARI.
SAMAHANI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA SIKU ZA NYUMA.
UKWELI NA UHAKIKA
SAMAHANI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA SIKU ZA NYUMA.
UKWELI NA UHAKIKA
Ijumaa, 17 Januari 2014
MFAHAMU MWANAMAPINDUZI CHE GUAVARA.
Ernesto Rafael
Guevara de la Serna au Che Guevara alizaliwa
tarehe 14. Mei 1928
Rosario, Argentina; 9. Oktoba 1967
La Higuera,
Bolivia alikuwa mtabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti
za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati
zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.
Wakati akisomea
utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani ya Kusini
ambapo alijionea mwenyewe umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha
ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi huku wachache wakiwa wanamiliki
mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa
njia pekee ya kuondoa umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi.
Aliamua kusoma
kwa undani falsafa za Karl Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati za
kisoshalisti nchini Guatemala chini ya rais Jacobo
Arbenzi Guzmán.Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la kijeshi
lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini Cuba mwaka 1959. Guevara alikuwa
mmoja wa viongozi wa serikali mpya ya Cuba. Katika kipindi hiki, Guevara
aliandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita vya
msituni kwa nia ya kuondoa madarakani tawala za kibepari na kibeberu.Mwaka 1965
Guevara aliondoka nchini Cuba akielekea Kongo-Kinshasa ambayo hivi sasa inaitwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kwa siri kusaidia harakati za kuondoa utawala
uliokuwa ukiongozwa na vibaraka wa mataifa ya Magharibi chini ya Mobutu Sese Seko
baada ya kuuawa
kwa Patrice Lumumba.
Moja ya watu ambao walifanya kazi na Guevara alipokuwa nchini Kongo ni
aliyekuwa baadaye rais wa nchi hiyo, Laurent Kabila.
Guevara
aliondoka nchini Congo na kuelekea Bolivia ambapo alikamatwa mwaka 1967 na jeshi la
Bolivia likishirikiana na majasusi wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA. Baada ya
kukamatwa kwake aliuawa kinyama.
Baada ya kifo
chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya
kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda
kuivaa vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.
Imechapishwa kwa msaada kwa msaada Wikipedia
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)